MAHAKAMA ya Rwanda imeeleza kwamba makosa yanayomkabili Paul Rusesabagina ya ugaidi na mengineyo ni makubwa na kutokana na hilo ataendelea kubaki rumande kwa siku nyingine 30.

Mahakama hiyo imemnyima dhamana Rusesabagina, ambaye hadithi yake wakati wa mauaji ya halaiki nchini humo, ilifanyiwa filamu ya hotel Rwanda.

Rusesabagina, ambaye ni raia wa Ubelgiji amekuwa akimkosoa rais Paul Kagame, anakabiliwa na mashitaka 13 ikijumuisha kufadhili ugaidi, kushiriki katika mauaji, kuandikisha wanajeshi watoto, na kuunda kundi la uasi.

Kama atakutwa na hatia huenda atakabiliwa na kifungo cha miaka 25 gerezani. Haijulikani ni lini kesi yake itasikilizwa tena.