KIGALI,RWANDA

SERIKALI  ya Rwanda imepokea  jumla ya magari ya wagonjwa 40 kutoka Ufalme wa Ubelgiji katika hatua inayolenga kuongeza huduma za matibabu nchini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Waziri wa afya Dkt.Daniel Ngamije alibainisha kuwa msaada huo unachangia kupatikana kwa mkakati wa kitaifa wa nchi hiyo katika muktadha wa kukabiliana na magonjwa ya miripuko ikiwa ni pamoja na Ebola na janga la corona na mengineyo.

“Hatua hii itaongeza ajenda ya maendeleo endelevu ya Rwanda kwa ustawi wa kijamii na kiuchumi wa watu wake. Kwa kuongezea, pia inaleta faida kwa kazi inayoendelea kuhakikisha Usalama wa Afya kwa Wote.”Waziri Ngamije alisema.

Kila ina thamani ya Rwf43 milioni, lakini Waziri alisema kuwa nchi hadi sasa imepokea jumla ya magari ya wagonjwa 43 kutoka Wabelgiji yenye thamani ya Rwf2 bilioni tangu mwanzo wa mwaka.

Ngamije alisema,Serikali ya Ubelgiji inasaidia sekta ya afya ya Rwanda katika miradi anuwai ambayo imekuwa ikisaidia sekta ya afya kuboresha upatikanaji wa huduma ya msingi ya afya.

Baadhi ya mipango hiyo ni pamoja na ujenzi wa Awamu ya kwanza ya Hospitali ya Wilaya ya Nyarugenge, Ujenzi wa Vituo vya Afya huko Kigali .

Balozi wa Ubelgiji nchini Rwanda Benoit Ryelandt aliunga mkono maoni hayo akisema msaada huo ulipangwa kupanua na kuwezesha upatikanaji wa huduma za afya,hasa kwa faida ya watu wanaoishi vijijini.

Hata hivyo Ryelandt alisema kwa kuzingatia mahitaji ya dharura ya usafirishaji wa matibabu ambao pia uliharakishwa kutokana na janga la Covid-19, wanaweza kupitia ununuzi wa haraka na kutoa gari zote za wagonjwa 40 mara moja.