NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM
MGOMBEA Mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan, amewataka wakaazi wa Dar es Salaam kupiga kura za kutosha kuanzia ngazi ya urais, wabunge na madiwani, ili kundelea kuwaletea maendeleo.


Akizungumza juzi jijini humo,wakati wa kuomba kura kwa wananchi Samia, alisema CCM inafanya maendeleo na hairudi nyuma.


Alisema wamejipanga kuendele kuleta maendeleo katika jiji hilo, kuweka nguvu maalum Jangwani, kwa kuwa eneo hilo limekuwa kero hasa kipindi cha mvua zinaponyesha, nakuwekeza katika ujenzi wa barabara ya mwendokasi katika maeneo mbalimbali.
Alisema eneo la Jangwani limekuwa na kero hivyo hakuna lazima kuondoa changamoto hizo kwa kuwa tunataka shida hizo zisaulike.


Alitaja baadhi ya barabara zinazotarajiwa kujengwa ni Samnujoma hadi Mwenge, Morocco na Mwaikibaki ndani ya mwaka ujao pamoja na daraja la Salenda .
Aliongeza kuwa Chama cha CCM kinaendesha kampeni zake kwa jitihada zake na kwa kutumia Ilani ya Chama, sio kama chama fulani kinachoenda Ubeligiji kufundishwa maneno hivyo kazi kwao.


Alieleza kuwa mgombea Urais CCM Dk. Magufuli anawashukuru sana kwa imani na ushirikano walionyesha kwa wana Dar es Salaam kwa kuwwa bega kwa miaka mitano iliyopita .
Pia anawashukuru hata pale alipotekeleza agizo la CCM ,Serikali kuamia mjini Dodoma wana Dar es Salaam wametoa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza hilo.


Aliongeza kuwa mbali na maendeleo mengine ,pia Serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 18 za dawa na vitendea kazi, na hiyo ndio kazi iliyofanywa na waliokotwa majalalani
Naye mgombea Ubunge wa jimbo la Temeke Doroth Kilambe aliomba kura za Urais, Ubunge na Udiwani kupigwa za kutosha ndani ndani ya chama hicho.


Kwa upande wa Mgombea wa jimbo la Ubungo Profesa Kitila Mkumbo alibainisha jiji la Dar es Salaam linapata maji kwa asilimia 88 huku huduma za afya zikiimarika kwa kiasi kikubwa.