LONDON, England

MCHEZAJI wa zamani wa Manchester United Alexis Sanchez amesema kwamba hakufurahia siku yake ya kwanza katika klabu yake baada ya kujiunga na Arsenal.

Sanchez ambaye amejiunga na Inter Milan baada ya msimu mmoja akihudumu kwa mkopo kutoka United, anasema kwamba alimuomba wakala  wake, iwapo angeweza kuvunja mkataba wake ili kurudi London, baada ya kuhamia Old Trafford katika uhamisho wa kubadilishana wachezaji mwezi Januari 2018.

”Mara nyengine kuna vitu ambavyo hutavijua hadi unapowasili”, alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 katika kanda ya video ya Instagram.”Kuna kitu ambacho sikuelewa na hakikuwa vizuri”.