NA BAKAR MUSSA, PEMBA
KAMATI ya maadili ya shehia ya Selemu Wete imepiga marufuku watoto kushirikishwa katika vitendo vya udhalilishaji, ikiwemo kufanyishwa kazi za kupara samaki huku wazazi wao wakaridhia hali hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi sheha wa Shehia ya Selemu ,Ali Khatibu Chwaya, alisema wimbi la udhalilishaji kwa watoto lilikuwa limeshamiri katika shehia yake na aliamuwa kuunda kamati hiyo
iliwashirikiasha watu wa aina mbali mbali.Chwaya , alifahamisha sababu kubwa iliofanikisha hilo ni kuondosha
tafauti za wananchi ikiwemo kuweka mbele itikadi za kisiasa na kuonakwamba suala la kupinga udhalilishaji wa watoto ni suala muhimu katika jamii.“ Tuliona hakuna sababu ya kuviacha vitendo hivi vikiendelea wakatitaasisi mbali mbali kama vile Wahamaza, Tamwa, wamekuwa wakichukuwa
juhudi mbali mbali za kutowa mafunzo ya kupinga udhalilishaji nikawakusanya wananchi nikawaeleza wakakubali nashukuru
tumefanikiwa,”alieleza.Haji Thabit Haji mwananchi wa shehia ya Selemu alikuwa likisumbuwa kwa watoto lakini kwa sasa limeondoka kwani wananchi wamekuwa wakifuatilia kwa umakini sana.