NA MWANDISHI WETU, MOROGORO 

CHAMA cha Mapinduzi, mkoa wa Morogoro kimesema Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Seif Sharif Hamad hana uwezo wa kuiunganisha Zanzibar kwa kuwa hana historia safi na aina ya siasa na uongozi wake hulenga kuwagawa wananchi.

Pia kimesisitiza na kumtaja kiongozi huyo sifa yake kubwa ni ubaguzi, ubinafsi na umimi ndiyo maana amekuwa na lundo la maadui toka akiwa mwanachama na kiongozi wa vyama vya ccm na cuf 

Hayo yameelezwa jana na katibu wa ccm mkoawa morogoro shaka Hamdu shaka akiwa ofisini kwake mkoani hapa kufuatia matamshi ya Maalim seif aliyesema akishinda atawaunganisha wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba.

Shaka alisema kabla ya Maalim seif kuwa kiongozi wa smz na ccm, zanzibar haikuwa na msamiati wa uunguja na upemba lakini toka ateuliwe kuwa waziri wa elimu na baadae waziri kiongozi smz, hapo ndipo misamiati ya upemba na uunguja ilipochipuka na kutamalaki kutokana na aina ya uongozi wake wa kibaguzi.

Alisema hapo zamani ukimsikia muunguja anamwita mtu mpemba au mpemba anamwita rafiki yake muunguja, ulikiwa ni sehemu ya utani na dhihaka isiyo na gharama lakini haukuwa na makali kama aliposhika nyadhifa za juu Maalim Seif.

“Si kweli kama Maalim Seif ana uwezo wa kuwaunganisha wazanzibari kama anavyojitapa. Umahiri na uwezo wake katika upinzani ni kuwagawa wananchi kwa asili, nasaba na rangi zao. Ni kiongozi mbaguzi, mbinafsi mwenye uwezo wa kuwagawa watu kwa mafungu”, alisema Shaka