KHATIB JUMA NAHODA

WANANCHI wa Wilaya ya Mkoani wametakiwa kutoa mashirikiano ya kutoataarifa kwa vyombo husika juu ya matendo ya kihalifu katika jamii

kabla na baada ya kutokea.Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya  kukaguwa  Migomba iliyohujumiwa kwa kukatwa katika Kijiji cha Minazini Kengeja Mkuu wa

Wilaya ya Mkoani ,Issa Juma Ali alisema wananchi wanapaswa kuwafichua wahalifu ambao wanahatarisha amani na usalama katika jamii.

Alisema kitendo cha kukatwa kwa Migomba katika shamba la Ali KhamisSaid (75) ni kitendo kinachoashiria uvunjifu wa amani hasa katika

kipindi hichi taifa likiwa katika kampeni za uchaguzi.’ Kitendo  hichi cha kukatwa kwa Migomba haya katika shamaba hili la

bwana Ali ni kiashiria cha uvunjifu wa amani’’ alielezaAlieleza  kitendo hicho kimetokea usiku wa tarehe 9/9/2020 na tukio

kama hili limetokea siku ya tarehe 28/08/2020 katika shamba ya MakameHababuu Ali, iliyopo Mtuhaliwa Wilaya ya Mkoani kwa Migomba 38 kukatwa.

Aidha  Mkuu huyo wa Wilaya alitembelea shamba la viazi vitamu  linalomilikiwa na Sheha wa shehia ya Kengeja ambalo usiku huo huo wa tarehe

9/9 sehemu ya shamba hilo liling’olewa.‘’ Uhalifu huu si mara ya kwanza kufika katika ofisi yangu, hili

limetokea tarehe 9/9 na kitendo chengine kimetokea 28/8/2020’’alisema. Alifahamisha kuwa kuna uwezekano mkubwa matukio hayo yanalenga chuki

za kisiasa kutokana na wafanyiwaji wa vitendo hivyo kuwa na itakadi ya Chama cha Mapinduzi.

’ Na haya matendo yanaashiria kuwa ni chuki za kisiasa kwa sababu alifahamisha. Sambamba na hayo aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya Upelelezi, ili muhusika afikishwe katika vyombo vya sharia.