NAIROBI, Kenya

JOPO la usuluhishi wa migogoro ya michezo nchini Kenya (SDT) limetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na kampuni ya KPL inayoendesha Ligi Kuu ya Kenya, ikipinga maamuzi ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kumaliza michezo ya Ligi Kuu ya msimu wa 2019-20 na kutawaza Gor Mahia mabingwa.

Katika maamuzi yake, Mwenyekiti wa SDT John Ohaga alisema kwamba Ofisa Mkuu wa KPL Jack Oguda, hakutafuta njia nyingine za kupata suluhu kati ya KPL na FKF kabla ya kushtaki shirikisho kwa SDT.

Ohaga pia aliamua kwamba Oguda, ambaye alikuwa mlalamikaji katika kesi hiyo, aliwasilisha mashtaka bila ya kuwa na idhini kutoka kwa timu za Ligi Kuu ya soka ya Kenya.