NA ARAFA MOHAMED
WAFANYABIASHARA wa mnada wa samaki waliopo katika maeneo ya Bwawani msikiti mabuluu Mjini Unguja, wametakiwa kuendelea kuuza bishara zao katika sehemu hiyo waliowekwa hadi pale Serikali itakapo toa tamko .
Afisa Uhusiano wa Baraza la Manispaa Mjini Seif Ali Seif, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili Ofisini kwake Malindi mjini Unguja.
Alisema wauza samaki hao walioondolewa katika soko la Darajani na kupelekwa Mlandege Mskiti Mabluu, kutokana na kupunguza msongomano baada ya kuibuka kwa maradhi ya Corona, hivyo aliwataka wafanyabiashara hao kuendelea kubaki.
Aidha Seif, alisema kuwa kutokana na maradhi ya corona yalipoingia nchini kulikuwa hakutakiwi msongamano wa watu ndipo wakapunguzwa wafanyabiashara wa masoko mbalimbali kwa upande wa wauza samaki Darajani.
“Wafanya biashara wa soko la samaki Darajani waliopunguzwa na kupelekwa Mlandege waendelee kubaki hapo walipowekwa mpaka pale litakapotoka tamko kutoka Serikalini la kuwaweka Sehemu nyengine ”.alisema