RAIS wa Somalia, Mohamed Farmajo na viongozi watano wa majimbo wamemaliza mkutano wa siku tano huko Mogadishu, ambapo wamekubaliana kuhusu marekebisho ya mfumo wa uchaguzi.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na ofisi ya rais Farmajo imesema, serikali na majimbo watateua tume za uchaguzi za ngazi ya taifa na za kikanda kusimamia uchaguzi huo.

Viongozi hao pia wamesema hakutakuwa na vyama vya siasa vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi huo na uchaguzi huo utaanza Novemba 1 mwaka huu na serikali kuu na serikali za majimbo zitahakikisha usalama kwenye kipindi cha uchaguzi.