BARCELONA, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Barcelona Luis Suarez amekubali kujiunga na Juventus , kwa mujibu wa ripoti za mwandishi wa BBC radio 5 Live Guillem Balague.

Suarez atajiunga na mabingwa hao wa Serie A kwa uhamisho wa bila malipo au dau la kawaida iwapo ataweza kuondoka kutoka klabu hiyo.

Raia huyo wa Uruguay ana mwaka mmoja katika mkataba wake aliosaini 2016, lakini iwapo alicheza asilimia 60 ya mechi zote katika msimu wa 2020-21 ataongezwa mwaka mmoja zaidi. Suarez atafurahi kuondoka akiwa na msimu mmoja uliosalia.