ZASPOTI

MSHAMBULIAJI, Luis Suarez, amejikuta akishindwa kuzuia hisia zake alipotakiwa kutoa neno
moja tu la kwa heri kwa Barcelona, akajikuta akimwaga chozi kabla ya kurudi tena kwenye mazungumzo.


Suarez ameondoka Barcelona huku akiwa bado anahitaji kubakia, lakini, hakuwa na namna baada ya kocha mpya wa klabu hiyo, Ronald Koeman, kumtaka aondoke.
Akitoa neno la mwisho kwa wachezaji wenzake aliyoishi nao akina Lionel Messi, Jordi Alba, Gerard Pique, Sergio Roberto na Sergi Busquets, Suarez aliwataka Barca wajipange.


Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay ametimkia Atletico Madrid baada ya miaka sita ya kucheza Nou Camp.(AFP).