DAMESKI,SYRIA
NDEGE za kivita zimerusha makombora viungani mwa mji wa kaskazini mwa Syria, Aleppo jana.
wakati mashambulizi ya angani yakiongezeka nchini humo katika wiki za karibuni.
Hakukuwa na ripoti za haraka kuhusu hasara iliyotokea,mnamo Agosti 31, shambulizi la angani lilivilenga viunga vya mji mkuu Damascus na kuwawua wanajeshi wawili na kuwajeruhi wengine saba.
Israel huwa haizungumzii ripoti za aina hiyo,lakini inaaminika kuwa ilifanya mashambulizi kadhaa yanayolenga uwepo wa jeshi la Iran nchini Syria. Katika miezi mitatu pekee iliyopita,Syria iliituhumu Israel kwa kufanya karibu mashambulizi tisa ya angani kwenye mipaka yake.