NA MARYAM SALUM, PEMBA

KATIBU Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar, Mwita Mgeni Mwita amesemakuwa taasisi binafsi zina mchango mkubwa katika kuinua pato la Taifa kupitia mipango na mikakati ya maendeleo endelevu nchini na kwa maslahi ya Taifa.

Aliyasema hayo huko katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha ulioko GombaniChake Chake, wakati  akizungumza na taasisi mbali mbali zisizokuwa za

kiserikali zilizojumuika katika mkutano wao wa kujadili na kuchangiajuu ya suala zima la mpango wa maendeleo endelevu nchini.

Alieleza kuwa ili mpango huo wa maendeleo endelevu nchini uweze kuweponi lazima taasisi husika ziweze kutoa mchango mkubwa, ili kuinua pato

la Taifa kwa maslahi ya jamii.Alisema kuwa Tume hiyo imeandaa mpango wa makusudi wa kukusanya

taasisi hizo kwa pamoja katika mkutano huo, lengo ni kutoa michangoyao kama taasisi binafsi, ili michangio hiyo iweze kufanyiwa kazi na

lengo liweze kufikiwa kwa watu wote.“Lengo na dhamira kuu ya kukuiteni katika mkutano huu, ni kuona sisi

Tume ya Mipango tunapata mawazo mbali mbali kutoka kwenu ili tuwezekuiunganisha pamoja , ili  lengo letu liweze kufikiwa kwa maslahi yajamii na sio kwa maslahi yetu kama Tume ya Mipango,” alisema.