NEW DELHI, INDIA

JENGO la Taj Mahal nchini India limefunguliwa tena kwa watalii ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miezi sita, licha ya taifa hilo kuwa la pili kwa maambukizi ya virusi vipya vya Corona duniani.

Serikali ya India iliendelea kuregeza pole pole vikwazo vya shughuli za kiuchumi na usafiri wa watu ili kuwezesha uchumi kusonga mbele.

Hii ni licha ya kuwepo kwa jumla ya takriban visa 90,000 vya virusi vya korona kwa siku.

Taj Mahal ni jengo la kaburi lililojengwa katika karne ya 17 na mfalme Mughal kama kumbukumbu ya mkewe.

Jengo hilo linavutia watu takribani milioni saba kila mwaka,lakini lilifungwa katikati ya mwezi Machi mwaka huu kufuatia janga la corona.

Idadi ya watalii wanaoruhusiwa kufika hapo kwa siku imepunguzwa hadi 5,000.

Wanalazimika kuvaa barakoa na hawaruhusiwi kupiga picha za makundi makubwa.