NA SAIDA ISSA, DODOMA
KITUO cha taarifa kwa wananchi (TCIB) kimeaanda muongozo wa kuwasaidia wabunge katika kusimamia maamuzi mbalimbali yanayofanywa na serikali katika utekelezaji wa miradi ya umma.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dodoma na meneja mradi wa kituo hicho, John Kitoka mara baada ya kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa masuala ya manunuzi kuhusiana na masuala ya manunuzi na mikataba ya umma.
Kitoka alisema kutokana na utafiti mdogo walioufanya wamebaini kuwa wabunge wengi kutojua taratibu na kanuni na sheria za usimamizi wa umma, hivyo itawasaidia kuwaongezea maarifa katika kuisimamia serikali pamoja na kuihoji juu ya miradi mbalimbali inayoitekeleza.
“Muongozo huu utawasaidia waheshimiwa wabunge kuwafumbua macho na kuweza kuihoji serikali namna mbalimbali wanavyotekeleza miradi ya umma kwani wao ndio wawakilishi wa wananchi hivyo ni vizuri wananchi wakawa wanajua masuala ya maendeleo yanavyofanyika,” alisema