ZASPOTI
SHIRIKISHO la Soka Tanzania ( TFF), limesaini mkataba na Kampuni ya Six International Ltd ili kujenga vituo bora nchini katika kuendeleza soka na kufikia hadhi ya kimataifa.
Zoezi hilo la kusaini makubaliano hayo ya ujenzi wa vituo hivyo limefanyika jijini Dar es Salaam katika ofisi za TFF.


Makubaliano hayo yamelenga mradi huo utakaotekelezwa katika maeneo ya Kigamboni na Tanga.
Mradi huo utajengwa kwa kutumia fedha za FIFA na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12.
Rais wa TFF, Wallace Karia, alisema, miradi hiyo inakwenda kwa awamu na matarajio yake ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na vituo hivyo vya mpira.


“Mradi unakwenda kwa awamu, tutatumia fedha za wadau wetu mbalimbali pamoja na wale watakaojitokeza pia”, alisema, Karia.