BANGKOK,THAILAND

SERIKALI ya Thailand imeamua kurefusha hali ya dharura hadi mwishoni mwa mwezi Oktoba ikitaja kuwepo haja ya kuzuia ueneaji wa virusi vya Corona.

Serikali hiyo ilitangaza hali ya dharura iliotakiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Septemba itarefushwa hadi mwishoni mwa mwezi ujao.

Hali ya dharura ilitangazwa mara ya kwanza mwezi Machi na hii ni mara ya sita itakuwa inarefushwa.

Kwa kipindi cha miezi mitano iliyopita,idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona mara nyingi imepungua hadi chini ya kumi nchini Thailand.

Urefushwaji wa hali ya dharura ulisababisha mashaka hasa miongoni mwa vijana kwamba unalenga kuzuia maandamano dhidi ya serikali.

Maandamano ya kuipinga Serikali yameendelea katika miezi ya hivi karibuni.Waandamanaji wamekuwa wakitoa wito wa marekebisho ya katiba na mabadiliko ya ufalme wa Thailand.