NA ABOUD MAHMOUD

JUMLA ya timu sita za mchezo wa Netiboli visiwani Zanzibar zinatarajia kushiriki mashindano ya klabu Bingwa Tanzania ya mchezo huo, yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 28 mpaka Disemba 6 mwaka huu Mkoani Tanga.

Akizungumza na Zanzibar Leo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Netiboli Zanzibar (CHANEZA) Mkemimi Muhina Seif, alizitaja timu ambazo zitashiriki mashindano hayo kwa wanawake ni KVZ, Mafunzo, JKU na Zimamoto kwa upande wa wanaume ni timu mbili ambazo ni KVZ na JKU.

Alisema mbali na timu hizo timu ya Afya ya wanaume inatarajiwa kushiriki mashindano hayo ingawa mpaka hivi sasa bado hawajathibitisha ushiriki wao .

“Baada ya kukamilika kwa mashindano ya ligi kuu hivi sasa macho yetu wapo katika klabu bingwa Tanzania ambayo yanashirikisha timu za hapa visiwani na Tazania Bara,”alisema.