LONDON,UINGEREZA

WATU 400,000 hufariki kila mwaka katika mataifa ya Umoja wa Ulaya kutokana na hewa chafu. Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika la mazingira la Ulaya mjini Kopenhagen.

Utafiti huo unaeleza kuwa uchafuzi wa hali ya hewa ni kitisho kikubwa kwa mazingira katika eneo hilo. Shirika hilo limeleza pia kuwa, katika miaka 30 iliyopita hali imekuwa bora zaidi.

Katika miaka ya 1990 idadi ya waliofariki kutokana na kuchafuiliwa kwa hewa ilifikia watu milioni moja.Ripoti ya shirika hilo ilieleza pia kuwa kelele zinachukua nafasi ya pili katika kusababisha vifo vya watu zaidi ya 12,000.