COLOMBO, SRI LANKA
JESHI la Wanamaji la Sri Lanka limesema kuwa timu ya watu watatu waliokuwa kwenye meli ya mafuta ya MT New Diamond ambayo iliwaka moto katika pwani ya mashariki mwa Sri Lanka wiki iliyopita wameanza kufanya uchunguzi baada ya moto kuzimwa kabisa.
Timu hiyo kwa kusaidiana na wataalamu wa nje sasa imeshaanza kazi ya kutathmini hatua ya ajali hiyo iliyvyotokea sambamba na kupanda juu ya tanki la mafuta baada ya timu ya washiriki sita kutoka ng’ambo pia kusaidiana katika ukaguzi huo.
Jeshi la wanamaji lilisema uchunguzi wa awali juu ya meli hiyo iliyokuwa na tatizo tayari umekamilika.
MT New Diamond imebeba tani 270,000 za mafuta ilikuwa ikielekea Bandari ya Paradip nchini India kutoka Kuwait wakati moto ulipotokea katika chumba cha injini yake Alhamisi iliyopita, ikitishia kusababisha umwagikaji mkubwa wa mafuta katika Bahari ya Hindi mashariki mwa Sri Lanka.
Taarifa ilisema kwamba kiraka cha mafuta kilichoonekana baharini ambapo meli ilikuwepo kilisababishwa na uvujaji kutoka kwenye matangi ya mafuta ya meli na sio matangi ya mafuta yasiyosafishwa.
Meli hiyo kwa sasa iko maili 50 baharini kutoka pwani ya mashariki.
Jeshi la wanamaji liliongeza kwamba meli tisa kutoka Jeshi la Wanamaji la Sri Lanka, Walinzi wa Pwani ya India, na Jeshi la Wanamaji la India pamoja na Meli mbili za Walinzi wa Pwani ya Sri Lanka zilizopelekwa na wadau wengine zilikuwa wakishiriki kikamilifu katika operesheni hiyo.
Mbali na hayo, ndege za Jeshi la Anga la Sri Lanka na ndege ya Dornier ya Walinzi wa Pwani ya India wanafanya upelelezi wa anga mara kwa mara.
Hata hivyo, taarifa zilisema kuwa wataalamu hao kwa sasa wanaondosha gesi zenye sumu zinazosababishwa na moto, kutoka kwenye chumba cha injini na sehemu zingine za meli.