Edouard Mendy
CHELSEA imearifiwa kwamba lazima ilipe pauni milioni 30 kumsajili mlinda mlango wa Senegal, Edouard Mendy (28), kutoka Rennes. (Telegraph).

Sokratis Papastathopoulos
RAIS wa Napoli, Aurelio de Laurentiis, amesema wanataka kumsajili mlinzi wa Arsenal, Mgiriki Sokratis Papastathopoulos (32), hatua ambayo inaweza kutoa mwanya kwa Kalidou Koulibaly (29), kujiunga na Manchester City. (Standard).

Chris Smalling
MLINZI wa Manchester United, Chris Smalling (30), anaonekana kuwa tayari kujiunga na Roma kwa mkataba wa kudumu. (Mirror).

Sergio Reguilon
KLABU ya Sevilla ina matumaini ya kuendelea kuwa na beki wa Real Madrid, Sergio Reguilon (23) kwa mkopo kwa msimu mwengine licha ya Muhispania huyo kuhusishwa na uhamisho wa kudumu hadi Manchester United. (Marca).

Dani Ceballos
ARSENAL inakaribia kukamilisha makubaliano ya mkopo ya kumsajili kiungo wa Real Madrid na Hispania, Dani Ceballos kwa msimu wa pili kufuatana. (Mail).

Felipe Anderson
KLABU ya Arsenal inafikiria kumtafuta kiungo wa kati wa West Ham, Mbrazil, Felipe Anderson (27). (Football Insider).

Harry Wilson
LIVERPOOL haitakubali kiungo wa kati wa Weles, Harry Wilson (23), kuondoka tena kwa mkopo licha ya Newcastle, Leeds na Southampton kuonesha nia ya kumtaka.(Goal).

Ivan Perisic
INTER Milan itahitajika kutafuta fedha kwa kumuuza kiungo wa kati wa Croatia, Ivan Perisic ikiwa itataka kutoa ofa kwa mchezaji wa Chelsea na kiungo wa Ufaransa, N’Golo Kante (29). (Gazzetta dello Sport).

Jean-Claude Billong
KLABU za Crystal Palace, West Ham, West Brom, Norwich na Watford zinamnyatia mlinzi wa Ufaransa, Jean-Claude Billong (26), anayecheza katika ligi ya ‘Serie B’ Salernitana. (Teamtalk).

Krzyszt Piatek
AS Roma inafikiria kumchukua mshambuliaji wa Hertha Berlin na Poland, Krzyszt Piatek kuchukua nafasi ya Edin Dzeko. (Gazzetta dello Sport).

Alfie Jones
KLABU ya Hull City inataka kumsajili beki wa kati wa Southampton, Alfie Jones (22), kwa mkataba wa kudumu. (Yorkshire Post).

Javi Martinez
KIUNGO wa Bayern Munich, Muhispania Javi Martinez (32), amedhamiria kufikia makubaliano kurejea Athletic Bilbao msimu huu. (Goal).