AURELIO DE LAURENTIIS

RAIS wa Napoli Aurelio de Laurentiis amesema beki kutoka  Senegal Kalidou Koulibaly, 29, ataondoka kwa bei nzuri msimu huu, huko Manchester United na Manchester City wakiongoza kwenye kumuwania. (Talksport)

KOULIBALY

MANCHESTER CITY inajipanga kuweka mambo sawa kutuma ofay a pauni milioni 66 kumsaini Koulibaly wiki ijayo. (Inside Futbol)

TIMO WERNER

MSHAMBULIAJI mpya wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 24, alikataa kuhamia Manchester City baada ya Pep Guardiola kumwita kuzungumzia uwezekano wa kuhamia. (Mail)

JAMES TARKOWSKI

WEST HAM wanataka kutoa zaidi ya euro milioni 20 kwa beki wa kati wa Burnley Mwingereza James Tarkowski, 27. (Sky Sports)

MEMPHIS DEPAY

BARCELONA imekubali kumsaini winga Memphis Depay, 26, kutoka Lyon. (Teamtalk)

JADON SANCHO

MANCHESTER UNITED wamejiandaa kujaribu kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, kwani wanahisi hesabu ya klabu hiyo ya Ujerumani kwa mchezaji huyo wa miaka 20 ni kubwa mno. (Star)

RYAN FRASER

WINGA wa Scotland Ryan Fraser amewasili Tyneside kwa kufanya mzungumzo na Newcastle United. Mchezaji huyo miaka  26 kwa mujibu wa wakala wake yupo huru baada ya kuondoka Bournemouth. (Sky Sports)

THOMAS PARTEY

ARSENAL wamewapeana wachezaji wawili wawili wa Ufaransa Matteo Guendouzi na Alexandre Lacazette, kwa makubaliano ya kubadilishana na kiungo wa kati wa Ghana na Atletico Madrid, Thomas Partey. (Mirror)

CRYSENCIO SUMMERVILLE

LEEDS wanafanya mazungumzo na Feyenoord juu ya mshambuliaji Crysencio Summerville, na kijana huyo wa miaka 18 “kuruhusiwa kuondoka” klabu cha Uholanzi kuelekea Elland Road. (Leeds Live)

BRENTFORD OLLIE WATKINS

ASTON VILLA wamefanikiwa katika mazungumzo juu ya makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford Ollie Watkins, 24. (Football Insider)