RYAN FRAZER

MCHEZAJI wa Scotland Ryan Frazer 12 amekubali kujiunga na klabu ya Newcastle baada ya kuondoka klabu ya Bournemouth mwisho wa msimu na sasa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya matibabu. (Sky Sports)

RONALD KOEMAN

KOCHA  mpya wa Barcelona Ronald Koeman ameambia klabu hiyo anataka kumzuia Phillipe Coutinho msimu huu badala ya kumtoa mchezaji huyo wa Brazil kwa mkopo. (Marca)

OLE GUNNAR SOLSKJAER

KOCHA wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amezungumza na winga wa England Jadon Sancho, 20, kuhusu kujiunga na klabu hiyo kutoka klabu ya Borussia Dortmund msimu huu . (Express)

GARETH BALE

LICHA ya Gareth Bale kutaka kuondoka Real Madrid , klabu hiyo haijapokea maombi yoyote ya mshambuliaji huyo wa Wales, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 akikataa kupunguziwa mshahara wake na hivyobasi kuwazima wanaommezea mate. (Mundo Deportivo – in Spanish)

EDIN DZEKO

MSHAMBULIAJI wa Bosnia Edin Dzeko, 34, ameomba kuondoka klabu ya Roma na kujiunga na Juventus. (Corriere dello Sport – in Italian)

LAUTARO

Barcelona inaandaa ofa ya mwisho kumnunua mshabuliaji wa Argentina Lautaro , 23. (Goal)

JAMES TARKOWSKI

WEST HAM italazimika kuongeza ombi lao la dau la pauni milioni 27 ili kuwa na fursa yoyote ya kumsajili beki wa kati wa Burnley James Tarkowski, 27. (Sun)

JAYDEN BOGLE

SHEFFIELD UNITED inakamilisha dau la pauni milioni 11 kumsaini beki wa Derby na England Jayden Bogle, 20, na Max Lowe, 23, na pia watampeana mshambuliaji wa Ireland Callum Robinson, 25, ili kumpata winga wa Usochi Oliver Burke, 23. (Mail)

SHEYI OJO

MCHEZAJI wa Liverpool na aliyekuwa winga wa timu isiozidi wachezaji wa miaka 21 nchini England Sheyi Ojo, 23, anatarajiwa kujiung na klabu ya Cardiff katika ligi ya daraja la kwanza nchini England kwa mkopo licha ya hamu kutoka Nottingham Forest. (Liverpool Echo)