Julian Draxler
KLABU ya Leeds United inajaribu kumshawishi kiungo wa Paris St-Germain na Ujerumani, Julian Draxler (26), ajiunge na klabu hiyo. (RMC Sport).

John Stone
BEKI wa kati raia England, John Stone (26), anajiandaa kubakia Manchester City msimu huu na kupambania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Pep Guardiola. (Telegraph).

Fikayo Tomori
BEKI wa Chelsea na England, Fikayo Tomori (22), anakaribia kutua Everton kwa mkopo wa muda mrefu. (ESPN).

Eric Garcia
KLABU ya Barcelona ipo tayari kufufua tena nia yao ya kumsainisha beki wa Kihispania wa Manchester City, Eric Garcia (19). (Mundo Deportivo).

David Brooks
LEICESTER City inaonekana kuizidi kete Manchester United kupata saini ya winga wa Bournemouth na Wales, David Brooks (23). (Manchester Evening News).

Sergio Romero
KLABU ya Manchester United ipo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kipa wao Muargentina, Sergio Romero (33), ambapo Aston Villa na Chelsea zinaripotiwa kumtaka. (Express).

Rhian Brewster
LIVERPOOL inafikiria kumuuza msimu huu mshambuliaji wa timu ya taifa ya chini ya miaka 21, Rhian Brewster (20), kwa sharti la kumrejesha tena siku za usoni. (Sky Sports).

Alphonse Areola
KLABU ya Arsenal imepewa ofa ya kumsajili kipa wa Ufaransa, Alphonse Areola (27), kwa mkopo wa muda mrefu kutoka Paris St-Germain. (Mirror).

Emiliano Martinez
KLABU ya Aston Villa inataka kukamilisha haraka usajili wa kipa Muargentina, Emiliano Martinez (28) kutoka Arsenal ili awahi kucheza mechi ya ya kufungua msimu. (Mail).

Andre Gray
KLABU ya West Brom inafikiria kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Watford na Uingereza, Andre Gray (29). (Mail).

Conor Gallagher
KLABU ya West Brom na Leeds zimeongeza nguvu kwenye nia yao ya kumsani kwa mkopo kiungo wa Chelsea na England Conor Gallagher (20). (Mail).

Cameron Carter-Vickers
KLABU ya Bournemouth imepeleka ofa ya kumsajili kwa mkopo beki wa Tottenham na Marekani, Cameron Carter-Vickers (22). (Football Insider).