Hector Bellerin
BARCELONA imewasiliana na Arsenal kuhusu uhamisho wa beki wa kulia Muhispania Hector Bellerin (25). (Sport).

Gareth Bale
REAL Madrid wapo tayari kulipa nusu ya mshahara wa mwaka wa Gareth Bale ili kusaidia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 raia wa Wales kuondoka Bernabeu.(Telegraph).

Moise Kean
MSHAMBULIAJI wa Everton na Italia, Moise Kean (20), anataka kurudi Juventus, klabu aliyotoka kabla ya kujiunga na ‘Toffees’ mwaka 2019. (Calciomercato).

Edouard Mendy
KLABU ya Rennes imethibitisha wapo kwenye mazungumzo na Chelsea kwa ajili ya mlinda mlango Msenegali, Edouard Mendy (28). (Goal).

Phil Foden
MENEJA wa England, Gareth Southgate atafanya mazungumzo na kiungo wa Manchester City, Phil Foden (20), na mshambuliaji wa Manchester United, Mason Greenwood (18), baada ya nyota hao kuvunja masharti ya ‘corona’ wakiwa na timu ya taifa. (Mail).

Matt Richie
KLABU ya Bournemouth inataka kumsainisha kiungo wa pembeni wa Scotland na Newcastle, Matt Richie, lakini, wamekwama kukubaliana na masharti binafsi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Newcastle Chronicle).

David Luiz
BEKI wa kati wa Arsenal na Brazil, David Luiz (33), huenda akaukosa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa msimu huu kufuatia maumivu ya shingo. (Telegraph).

Joshua King
ASTON Villa inataka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway, Joshua King, lakini, nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 anapendelea zaidi kutua Manchester United baada ya uhamisho wake kwenda Old Trafford kukwama kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. (Athletic).

Alexandre Lacazette
MSHAMBULIAJI wa Arsenal na Ufaransa, Alexandre Lacazette (29), atatafuta ufafanuzi zaidi kuhusu majukumu yake kwenye timu wakati huu tetesi zikisema washika bunduki hao wanataka kumuuza msimu huu. (ESPN).

Emiliano Martinez
ASTON Villa imeongeza dau zaidi linalovuka pauni milioni 15 kwa ajili ya kumnasa kipa wa Arsenal Muargentina Emiliano Martinez (28), baada ya dau lake la kwanza kugonga mwamba. (Goal).

Troy Deeney
KLABU ya Watford haitamzuia mshambuliaji wake raia wa England, Troy Deeney (32), kutaka kurejea kukipiga Ligi Kuu ya England. (Mail).