JADON SANCHO

MANCHESTER UNITED wanafikiria kumaliza harakati zao za kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20. (Star)

SENEGAL ISMAILA

LIVERPOOL wanadhamiria kumsajili mshambuliaji wa Watford na Senegal Ismaila Sarr, 22, mnamo Januari. (Football Insider)

HECTOR BELLERIN

BARCELONA itatoa ofa ya mkopo kwa Arsenal kwa beki wa Uhispania Hector Bellerin, 25. (Marca – in Spanish)

EDOUARD MENDY

MLINDA mlango wa Rennes Edouard Mendy, 28, atapata matibabu huko London wikendi hii baada ya Chelsea kukubali makubaliano ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal. (Star)

OLIVIER GIROUD

MSHAMBULIAJI wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, “alishangaa” na uvumi unaomuunganisha na Juventus. (Telefoot, via Mail)

JAMES TARKOWSKI,

MENEJA David Moyes anasema West Ham haitakidhi bei ya mlinzi wa Burnley na timu ya taifa ya Uingereza James Tarkowski, 27. (Football London, via Lancs Live)

ARKADIUSZ MILIK

HUENDA Tottenham wakamsaini mshambuliaji wa Napoli na Poland Arkadiusz Milik, 26, wakati wa usajili wa sasa. (Sky Sports)

ROY HODGSON

MENEJA wa crystal Palace Roy Hodgson anasema anashangaa hakuna vilabu “vinavyobisha hodi” na njia rasmi za winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 27.(Standard)

TROY DEENEY

WEST BROM iko kwenye mazungumzo ya hali ya juu kumsajili mshambuliaji wa Watford na England Troy Deeney, 32. (Football Insider)