RONALD KOEMAN
MENEJA wa Barcelona Ronald Koeman anataka kumfanya mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 28, kuwa moja ya mchezaji anayetaka kumsajili.(Sunday Express)

GARETH BALE
MANCHESTER UNITED inaweza kufanya usajili wa winga wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 31, ikiwa na mabadala wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20. (Sunday Express)

SERGIO REGUILON
BEKI wa kushoto wa Hispania Sergio Reguilon, 23, angependelea kutolewa kwa mkopo Sevilla kuhamia Manchester United. (AS – in Spanish)

ANDREA BELOTTI
TOTTENHAM wamekataliwa ombi lao la mkopo kwa mshambuliaji wa Torino na Italia, Andrea Belotti, 26. (Sky Italia – in Italian)

BENOIT BADIASHILE
MANCHESTER UNITED inajiandaa kutoa pauni milioni 23 kwa mlinzi wa Monaco na Ufaransa Benoit Badiashile, 19. (L’Equipe, via Sunday Express)

ANTONIO CONTE
MENEJA wa Inter Milan Antonio Conte anamtaka beki wa kulia wa Chelsea na Hispania Marcos Alonso, 29, katika klabu yake ya ligi ya Serie A. (Sky Italia, via Mail on Sunday)

OLEKSANDR ZINCHENKO
KIUNGO wa kati wa Manchester City na Ukraine Oleksandr Zinchenko, 23, atakuwa tayari kuwa sehemu ya makubaliano ya kubadilishana kwa beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 29. (Radio Marte, via Sun)

YAYA TOURE
MCHEZAJI wa zamani wa Manchester City na Ivory Coast kiungo Yaya Toure, 37, hana mpango wa kustahafu na anataka kucheza ligi ya Serie A. Hivi yupo huru kwa mujibu wakala wake, baada ya kuachana na tmu ya China ya Qingdao Huanghai mnamo Januari. (Tuttomercato via Goal)

SOLLY MARCH
WEST HAM inavutiwa na winga wa Brighton 26 Solly March na wameanza mazungumzo. (90min)