DANNY INGS

TOTTENHAM inapenda kumpata mshambuliaji wa Southampton, Muingereza Danny Ings, 28. (Football.London)

GARETH BALE

MANCHESTER UNITED itapaswa kulipa kiasi cha pauni milioni 18.5 pekee ikiwa wanataka kumsajili winga wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 31.(Mundo Deportivo – in Spanish)

DOUGLAS COSTA

DOUGLAS COSTA amewekwa tayari kuuzwa na Juventus. Manchester United awali walikuwa wakihusishwa na taarifa za kumtaka winga huyo wa Brazil, 29. (Goal)

CHRISTIAN ERIKSEN

KIUNGO wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 28, anaweza kuruhusiwa kuondoka Inter Milan ikiwa ni miezi kadhaa tu tangu kujiunga akitokea Tottenham. (Calciomercato – in Italian)

RINAR RUNARSSON

ARSENAL inataka kumsajili mlinda mlango wa Iceland Rinar Runarsson, 25, na imeanza mazungumzo na Dijon kuhusu mpango huo. (Telegraph)

ALEX TELLES

PORTO imepunguza gharama ya kumnasa beki wa kushoto Mbrazili Alex Telles mpaka pauni milioni 18.5, huku Manchester United ikimtaka mchezaji huyo, 27. (A Bola – in Portuguese)

SERGIO REGUILON

TOTTENHAM inaweza kuchuana na Manchester United kupata saini ya Beki wa kushoto wa Real Madrid, Mhispania Sergio Reguilon,23. (Mail)

ALEXANDER SORLOTH

SPURS wako kwenye mazungumzo na Trabzonspor kwa ajili ya mpango wa kumpata mshambuliaji Alexander Sorloth. Mchezaji huyo, 24 anacheza kwa mkopo wa miaka miwili akitoka Crystal Palace. (Express)

CENGIZ UNDER

NEWCASTLE inataka kumchukua winga wa Roma na Uturuki Cengiz Under kwa mkopo. Leicester pia inavutiwa na mchezaji huyo wa miaka 23. (Inside Futbol)

DAVID BROOKS

BOURNEMOUTH imeiambia Leicester kuwa watapaswa kulipa pauni milioni 50 kumpata kiungo wa kati David Brooks, 23.(Sun)