Pierre-Emerick Aubameyang
MKATABA wa miaka mitatu wa mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang kuichezea Arsenal una thamani ya pauni milioni 55 yakiwemo marupurupu. (Times).

Dele Ali
KLABU ya Tottenham huenda wakamtumia kiungo wa kati wa England, Dele Alli (24), kama chambo wakati wakijaribu kumrejesha, Gareth Bale (31), kutoka Real Madrid. (Mail).

Theo Walcott
EVERTON huenda wakakubali ofa kwa ajili ya wachezaji kadhaa, akiwemo winga wa England, Theo Walcott (31), winga wa Nigeria Alex Iwobi (24), na mshambuliaji Muitaliano, Moise Kean (20), wakati wakitarajia kuongezea nguvu kikosi cha Carlo Ancelotti. (Mirror).

Thomas Partey
KLABU ya Arsenal bado wanapanga kuwaongeza wachezaji zaidi kwenye kikosi chao, huku wakiwalenga kiungo wa kati wa Atletico Madrid, Thomas Partey, 27 na kiungo mchezeshaji wa Lyon, Mfaransa Houssem Aouar (22), miongoni mwa wachezaji wanaowataka. (Mirror).

Callum Hudson-Odoi
KLABU ya Bayern Munich ipo tayari kurudisha shauku yao kwa ajili ya winga, Callum Hudson-Odoi (19), huku wababe hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa na matumaini kuwa Chelsea itapokea ofa yao.(Mail).

Eric Garcia
BARCELONA itajaribu kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Manchester City, Eric Garcia (19), msimu huu ikiwa wataweza kuwauza walinzi wa kati, Samuel Umtiti (26), na Jean-Clair Todibo (20). (Mail).

Luis Suarez
JUVENTUS wanakumbana na wakati mgumu kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez, ambaye anapata changamoto kupata pasi ya kusafiria ya Italia kwa haraka.(Goal).

Edourd Mendy
CHELSEA inaelekea ukingoni kukamilisha taratibu za kumsajili Msenegali, Edouard Mendy (28). (Star).

Emerson Palmieri
KLABU ya Inter Milan bado wanamshawishi kumpa mkataba wa kudumu beki wa Chelsea, Emerson Palmieri (26), lakini, West Ham pia inamtolea macho wakitaka akichezee kikosi hicho kwa mkopo. (Independent).

Chris Smalling
KUSHINDWA kwa AS Roma kukubaliana na Manchester United kuhusu ada ili kumpata beki wa kati, Chris Smalling kutaifanya klabu hiyo ya Italia kufikiria kuhusu mbadala wake. (Mail).

Folarin Balogun
ARSENAL imekataa ombi la Sheffield kumnyakua mshambuliaji, Folarin Balogun. Klabu hiyo inaaminika kutoa ofa ya pauni milioni tatu na marupurupu mengine, lakini, washika bunduki wanataka dili la karibu pauni milioni 15 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye miaka 19, ambaye amechezea vikosi vya vijana vya Marekani na England. (Mail).