Thomas Partey
KIUNGO mkabaji wa Atletico Madrid, Thomas Partey (27), ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Arsenal, lakini, klabu hiyo ya Hispania watamuuza tu iwapo dau la pauni milioni 45 litafikiwa.(Football.London).

Sergio Reguilon
MLINZI wa kushoto wa Real Madrid na Hispania, Sergio Reguilon (23), yupo katika kiwanja cha mazoezi cha Tottenham kwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na miamba hiyo ya Ligi Kuu ya England.(Evening Standard).

Carlo Ancelotti
KOCHA wa Everton, Carlo Ancelotti, anataka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea, Fikayo Tomori (22), lakini pia yuko tayari kuwaachia wachezaji kadhaa wakiwemo viungo, Gylfi Sigurdsson (31), na Fabian Delph (30).(Times).

Jose Gimenez
MANCHESTER City wanajiandaa kwa uhamisho wa mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Atletico Madrid, Jose Gimenez, ikiwa Napoli itakataa kushusha dau kwa ajili ya mlinzi wa kati, Kalidou Koulibaly (29). (Guardian).

Ahmad Traore
MANCHESTER United inaangalia uwezekano wa kumsajili winga wa kulia wa Ivory Coast, Amad Traore (18), kutoka Atalanta. (Manchester Evening News).

Cengiz Under
KLABU ya Leicester City wapo karibu kumsajili winga wa Roma, Cengiz Under.(Telegraph).

Ronaldo Koeman
Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amesema, timu hiyo haitamrejesha mlinzi wa Manchester City, Muhispania Eric Garcia (19). (Manchester Evening News).

Runar Runarsson
ARSENAL inamfuatilia mlinda mlango wa Dijon, Runar Alex Runarsson, 25, huku washika bunduki hao wakiwa na matumaini makubaliano ya dau la pauni milioni 1.5 litafikiwa. (Evening Standard).

Memphis Depay
RAIS wa Lyon, Jean-Michel Aulas amekana ripoti kuwa mchezaji wa nafasi ya kiungo wa kati, Memphis Depay, aliyekuwa akichezea Manchester United yuko njiani kujiunga na Barcelona. (Evening Standard).

Folarin Balogun
KLABU ya Sheffield United imemfuatilia mshambuliji wa Arsenal, Folarin Balogun (19), kocha Chris Wilder amethibitisha.(Yorkshire Post).

Florent Indalecio
KLABU ya Newcastle imemjumuisha kiungo mshambuliaji raia wa Ufaransa, Florent Indalecio katika majaribio. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyekua akikipiga na Saint-Etienne kwa sasa hana klabu. (Newcastle Chronicle).