Ismaila Sarr
KLABU ya Liverpool wamemfuatilia, Ismaila Sarr na kujadili suala lake na Watford, ambayo inataka pauni milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.
Sarr pia ametambulika na Manchester United kama mbadala ikiwa mpango wa kumnasa winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho utashindwa.(Independent).
Ivan Perisic
MANCHESTER United pia wanafikiria uhamisho wa winga wa Inter Milan, Ivan Perisic (31), Kingsley Coman (24) anayekipiga Bayern Munich na Douglas Costa kutoka Juventus. (ESPN).
Sami Khedira
KLABU ya Manchester United itamfuatilia kiungo wa Ujerumani, Sami Khedira (33) mara mkataba wake na Juventus utakapokwisha. (Sun).
Edouard Mendy
WAKALA wa Edouard Mendy amedai kuwa makubaliano yamefikiwa kwa ajili ya mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 28, anayekipiga katika klabu ya Rennes kujiunga na Chelsea. (Stades).
David Raya
KLABU ya Brentford amekataa ofa ya takriban pauni milioni 10 kutoka Arsenal kwa ajili ya mlinda mlango, David Raya (25). (Telegraph).
Danny Ings
KLABU ya Southampton imeaiambia Tottenham kuwa mshambuliaji, Danny Ings (28), hauzwi kwa dau lolote.(Mail).
Cengiz Under
LEICESTER City inakaribia kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Uturuki, Cengiz Under (23), kutoka Roma na mlinzi wa Burnley, James Tarkowski (27), bado anatolewa macho na Brendan Rodgers.(Sky Sports).
James Tarkowski
WEST Ham imebadili muundo wa ofa kwa ajili ya kumnasa James Tarkowski, lakini, ofa hiyo bado imekataliwa na Burnley.(Sky Sports).
Mbwana Samatta
WEST Brom wanajaribu kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta, kabla ya mchezaji huyo mwenye miaka 27, hajamaliza mchakato wa kuhamia Fenerbahce. (Sun).
Nathaniel Clyne
MLINZI wa zamani wa Liverpool, Nathaniel Clyne anafanya mazoezi na klabu ya Crystal Palace na anaweza kupata mkataba na klabu hiyo ya Selhurst Park . (Standard).