Kristoffer Ajer
AC Milan ipo tayari kuzindua ofa ya pauni milioni 15 kwa ajili ya mlinzi wa Celtic, Kristoffer Ajer.
Miamba hiyo ya ‘Serie A’ inatarajiwa kukamilisha azma yao kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wiki ijayo, baada ya kumbainisha kama mlengwa wa uhamisho mapema msimu huu wa joto.(Sky Sports).

Rhian Brewster
CHRIS Wilder amethibitisha kuwa Sheffield United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Rhian Brewster.
Brewster amekuwa akingojea kwa uvumilivu nafasi yake ya kuang’ara huko Anfield tangu kuhitimu kwa kikosi cha wakubwa mnamo 2017.(Goal).

Luka Jovic
KOCHA, Zinedine Zidane anataka Real Madrid kumtoa kwa mkopo mshambuliaji anayesumbuka, Luka Jovic.
Mshambuliaji huyo wa Serbia amejitahidi kubakia Santiago Bernabeu tangu ajiunge na ‘Blancos’ kutoka Eintracht Frankfurt kwa euro milioni 60 katika msimu wa joto wa 2019.(AS).

Max Aarons
KLABU ya Norwich City imekataa ofa mbili kutoka Barcelona kwa ajili ya Max Aarons.
Moja ya zabuni ya wababe hao wa Uhispania ilikuja kwa pauni milioni 20 pamoja na mafao ya beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 20, lakini, ‘Canaries’ wanashikilia ada ya juu.(The Athletic).

Houssem Aouar
RAIS wa Lyon, Jean-Michel Aulas, amedai, Arsenal wanasita kufikia thamani ya klabu ya Houssem Aouar.
Aouar ameibuka kama moja ya mali moto zaidi katika soka ya Ulaya baada ya mwaka mwengine mzuri katika uwanja wa Groupama.(Goal).

Diego Godin
MLINZI wa Inter, Diego Godin yuko mbioni kujiunga na Cagliari.
Beki huyo wa kimataifa wa Uruguay atasaini kandarasi ya miaka mitatu hapo Sardegna Arena yenye thamani ya euro milioni 2.5 kwa msimu.(Calcio Mercato).

Nelson Semedo
BARCELONA ipo wazi kumuuza, Nelson Semedo kwa klabu za Ligi Kuu ya England wakati wa dirisha la uhamisho la sasa.
Blaugrana wamepokea ofa kadhaa kutoka kwa klabu za Kiingereza kwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 26, na wanaweza kuwasha taa ya kijani ya kuondoka kwake mwishoni mwa wiki.(ESPN).

DeAndre Yedlin
KLABU ya Newcastle ipo tayari kuidhinisha kuondoka kwa DeAndre Yedlin.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yuko tayari kukamilisha uhamisho kwenda Besiktas kabla ya dirisha la uhamisho wa majira ya joto kufungwa mwezi ujao.(NBC).

Chris Smalling
KLABU ya Inter wamepanga kuuteka uhamisho wa Roma kwa ajili ya beki wa Manchester United, Chris Smalling.
Nerazurri wapo tayari kulipia mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, kwa kuwa wamemuona aking’ara kwa mkopo huko Stadio Olimpico msimu uliopita.(The Sun).

Javi Martinez
KLABU ya Athletic iko karibu kumsaini, Javi Martinez kutoka Bayern Munich.
Mchezaji huyo wa miaka 32 atarudi uwanja wa San Mames kwa kandarasi ya miaka miwili na chaguo la mwaka mmoja wa ziada. (Marca).