DELE ALLI

WACHEZAJI wa Tottenham walipigwa na butwaa baada ya kiungo wa timu hiyo na England, Dele Alli, anayehusishwa na mipango ya kuhamia Paris St-Germain, kuachwa kwenye kikosi kilichoshinda Jumapili hii dhidi ya Southampton. (Mail)

ANTONIO RUDIGER

MUSTAKABALI wa beki Antonio Rudiger katika timu ya Chelsea uko mashakani baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichofungwa Jumapili hii na Liverpool, licha ya kwamba Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 27 hana majeruhi (Mail)

MIKEL ARTETA

KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta anasema Klabu hiyo haiko kwenye mazungumzo na Alexandre Lacazette kuhusu mkataba mpya, mshambuliaji huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 29, amebakiza miaka miwili ya mkataba wake na klabu hiyo

SASSUOLO MARLON

FULHAM imetuma ofa ya kumnasa mlinzi wa Sassuolo Marlon, na kwa mujibu wa mkurugenzi wa klabu hiyo Giovanni Carnevali, mazungumzo yanaendelea kuhusu uhamisho wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports Italia, via Football Italia)

ALEX TELLES

BEKI wa Kibrazil Alex Telles, 27, amesisitiza kwamba lengo lake kwa sasa ni kuichezea Porto, licha ya kuhusishwa kwake na kuhamia Manchester United. (Sport TV, via Metro)

LUKE SHAW

MLINZI wa kushoto wa Manchester United na England Luke Shaw, 25, amesema klabu hiyo inapaswa kufanya usajili zaidi, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho cha Old Trafford. (TV2, via Manchester Evening News)

RHIAN BREWSTER

CRYSTAL PALACE inaongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa timu ya Liverpool, Rhian Brewster (20), huku vilabu vya Sheffield United na West Brom vikionyesha nia ya kumsajili nyota huyo wa timu ya vijana ya England ya chini ya miaka 21. (Mail)

ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN

LIVERPOOL haina mpango wa kumuuza kiungo wa timu hiyo na England Alex Oxlade-Chamberlain (27), anayehusishwa na timu ya Wolves. (Mirror)

KIM MIN-JAE

LEICESTER CITY inatarajiwa kuungana na Tottenham kutaka kumsajili beki wa Beijing Guoan na Korea Kusini Kim Min-jae, 23. (90min)

RAVEL MORRISON

KIUNGO wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, 27, anatarajiwa kujiunga na klabu ya ADO Den Haag ya Uholanzi, baada ya kutemwa na Sheffield United. (Omroep West, via Football Oranje)