Alex Telles
BEKI wa Brazil, Alex Telles (27), anataka kuondoka klabu ya Porto na kujiunga na Manchester United, ambao wanajaribu kushawishi kupunguziwa dau lake la pauni milioni 36.6. (Telegraph).

Sadio Mane
LIVERPOOL wanatazamiwa kumtumia mshambuliaji, Sadio Mane, kumshawishi mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Senegali, Kalidou Koulibaly ili atue klabuni hapo kutoka Napoli, licha ya Manchester City na Paris St-Germain kuonyesha nia ya kumsaini mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29. (Le Parisien).

Antonio Rudiger
KLABU ya PSG wanamtaka beki wa Chelsea, Mjerumani Antonio Rudiger (27), kwa mkopo wa msimu mzima. (Mail).

Chris Smalling
AS Roma wanatarajiwa kuweka ofa nyengine ya pili kwa ajili ya mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling (30), ambaye aliichezea timu hiyo ya ligi ya ‘Serie A’ kwa mkopo msimu uliopita. (Guardian).

Lucas Torreira
KLABU ya Atletico Madrid wanalenga kumsajili kiungo wa Arsenal na Uruguay, Lucas Torreira (23). (Mundo Deportivo).

Joe Rodon
WEST Ham wapo tayari kupambana na Manchester United kwa ajili ya kupata saini ya beki wa kati wa Swansea City na Wales, Joe Rodon (22). (Guardian).

Wesley Fofana
WEST Ham United imeweka ofa yenye thamani inayofikia pauni milioni 33 kwa ajili ya mlinzi wa kati wa Saint-Etienne, Wesley Fofana (19), ambaye anawaniwa pia Leicester City. (Sky Sports).

Harry Wilson
KLABU ya Burnley wapo kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu kumsajili winga wa wekundu hao na Wales, Harry Wilson (23). (Independent).

Wesley Hoedt
LAZIO imefikia makubaliano na Southampton kwa ajili ya mlinzi wa Uholanzi, Wesley Hoedt (26), kurejea kwenye klabu hiyo ya Italia kwa mkopo. (Sky Sport Italia).

Sergino Dest
BARCELONA na Bayern Munich zimeweka ofa ya kumsajili mlinzi wa kulia wa Ajax na Marekani, Sergino Dest (19). (Marca).

Mario Gotze
KLABU ya Bayern imewasiliana na Mario Gotze kuhusu kujiunga tena na miamba hiyo. Mshambuliaji huyo wa Ujerumani (28), ni mchezaji huru baada ya kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu uliopita. (Sport Bild).

Santiago Arias
MLINZI wa kulia wa Atletico Madrid na Colombia, Santiago Arias (28), amewasili Ujerumani kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na Bayer Leverkusen. (Marca).

Francesco Totti
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Italia, Francesco Totti anatarajiwa kurudi Roma kama mkurugenzi wao mkuu wa michezo. (Corriere dello Sport).