Max Aarons
BEKI wa Norwich City Muingereza, Max Aarons (20) amekubali mkataba wa miaka mitano kujiunga na Barcelona. (Sport).

Ousmane Dembele
MANCHESTER United wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Ousmane Dembele (23), kutoka Barcelona. (Daily Record).

Dele Ali
KLABU ya Paris St-Germain wana uhakika kwamba kiungo wa Tottenham Hotspurs na England, Dele Alli (24), anataka kujiunga na miamba hiyo kwa mkopo wa msimu mzima. (Mail).

Matteo Guendouzi
KIUNGO wa Arsenal na Ufaransa, Matteo Guendouzi (21), ameomba kuondoka klabuni hapo. (Tribal Football).

Arkadiusz Milik
KLABU ya Newcastle United wanamtaka mshambuliaji wa Napoli na Poland, Arkadiusz Milik (26). (Corriere dello Sport).

Tom Davies
Southampton wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati raia wa England, Tom Davies kutoka Everton. (Talksport).

Houssem Aouar
ARSENAL imepata mpinzani wa klabu inayoshiriki ligi ya mabingwa Ulaya, katika mbio zake za kumwania kiungo wa Lyon na Ufaransa, Houssem Aouar (22). (Telegraph).

Sergio Romero
MLINDA mlango wa Argentina, Sergio Romero (33), anataka kuondoka Manchester United. (Sun).

Antonio Rudiger
MLINZI wa Chelsea Mjerumani, Antonio Rudiger (27), anaangalia hatma yake klabuni hapo baada ya kuachwa kwenye kikosi cha kwanza. (Sky Sports).

Jonathan Tah
BEKI wa Bayer Leverkusen, Mjerumani Jonathan Tah (24), hayuko kwenye orodha muhimu ya wachezaji wanaowaniwa na Leicester City.(Kicker).

Ademola Lookman
FULHAM wanajaribu kumsajili kwa mkopo winga wa zamani wa Everton na Charlton, Ademola Lookman. Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa anachezea RB Leipzig. (Evening Standard).

Jesse Lingard
KIUNGO wa Manchester United na England, Jesse Lingard (27), hatajiunga na Tottenham licha ya kuhusishwa kwake kutaka kuhamia timu hiyo. (Athleti).

Sofiane Boufal
WINGA wa Southampton raia wa Morocco, Sofiane Boufal (27), anawaniwa na klabu ya Ufaransa ya Angers. (L’Equipe).