DECLAN RICE

KOCHA wa Chelsea Frank Lampard anahitaji klabu hiyo kujaribu kufanya usajili wa kiungo mkabaji wa West Ham United Declan Rice 21 ingawa hakuna dau lililotumwa. Usajili wa kiungo huyo kutokea kwa wagonga nyundo wa London kutamfanya Jorginho wa Chelsea na Italia kutua ndani ya Arsenal.(Mirror)

ANTONIO RUDIGER

PARIS ST-GERMAIN wanavutiwa kumsajili mlinzi wa kati wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 27, ambapo Chelsea wako tayari kumtoa kwa mkopo na sio kumuuza. (Telegraph – subscription required)

MILAN SKRINIAR

TOTTENHAM wako kwenye mazungumzo na kitasa wa Slovakia ambaye anakipiga kunako klabu ya Inter Milan Milan Skriniar, 25. (Sun)

CHRIS SMALLING

INTER MILAN wanaweza pia kumsajili beki wa kati wa England na Manchester United Chris Smalling 30 kama watashindwa kufikia dau la Mslovakia. (Football Italia)

JULES KOUNDE

SEVILLA wanatarajia ofa nyingine kubwa kutoka kwa Manchester City inayomhitaji beki wao Jules Kounde, 21. (ESPN)

HOUSSEM AOUAR

ARSENAL wametuma ofa ya pauni milioni 32 ya kumhitaji kiungo wa Lyon Houssem Aouar 22 ingawa klabu hiyo inahitaji kiasi cha pauni milioni 54. (RMC Sport, via Metro)

RHIAN BREWSTER

NYOTA wa Liverpool na England aliye chini ya miaka 20 Rhian Brewster, anavutiwa kutua Sheffield United licha ya klabu ya Aston Villa kuhitaji huduma ya kinda huyo.(ESPN)

TEUN KOOPMEINERS

LEEDS UNITED wanakaribia kumsajili kiungo wa Kiholanzi mwenye miaka 22, Teun Koopmeiners kutokea AZ Alkmaar. (Telegraph – subscription required)

KEPA ARRIZABALAGA

MENEJA wa Chelsea Frank Lampard anapanga kufanya mazungumzo na Kepa Arrizabalaga, 25, juu ya hatima yake hasa baada ya kusajiliwa kwa Mendy 28 kutokea Senegal na Rennes.(Star)

STEVE BRUCE

KOCHA wa Newcastle United Steve Bruce amesema hafikiria kumuuza mshambuliaji wake raia wa Brazil Joelinton, 24, majira haya (Mirror)