Houssem Aouar
RAIS wa Lyon, Jean-Michel Aulas, ametoa onyo kwa Arsenal juu ya Houssem Aouar, akidai ofa yao ya ufunguzi ya pauni milioni 32 kwa kiungo huyo ni ndogo.
Iliripotiwa kwamba Arsenal iliwasilisha ombi rasmi kwa Aouar juzi na Mfaransa huyo alifikiriwa kuwa wazi kwa uwezekano wa kuhamia Emirates. (Goal).
Edinson Cavani
KLABU ya Atletico Madrid bado inafikiria kumchukua mshambuliaji wa zamani wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani.
‘Los Rojiblancos’ hawajatolea nje ofa ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, licha ya kumnasa raia mwenzake wa Uruguay, Luis Suarez kutoka Barcelona.(AS).
Chris Smalling
KLABU ya Inter inaangalia uwezekano wa kumchukua beki wa Manchester United, Chris Smalling.
Nerazzurri itamlenga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kama mbadala wa Milan Skriniar ikiwa atakamilisha uhamisho uliopendekezwa kwenda Manchester City.(Gazzetta Dello Sport).
Luka Jovic
KLABU ya Eintracht Frankfurt ameipiga na chini nafasi ya kumsaini tena, Luka Jovic kutoka Real Madrid.
Mshambuliaji huyo wa Serbia alikuwa na hamu ya kurudi Deutsche Bank Park kwa mkopo, lakini, miamba hiyo ya Ujerumani haina nia ya kupanga makubaliano.(AS).
Jadon Sancho
ANDY Cole amesema anaelewa kusita kwa Manchester United kutumia fedha za uenda wazimu kwa Jadon Sancho, na bei yake ya pauni milioni 109 ilionekana kuwa kubwa katika hali ya hewa ya sasa.
Ufuatiliaji ulioweka kumbukumbu wa United juu ya Sancho umekuwa hadithi ya muda mrefu zaidi ya uhamisho wakati wa msimu wa joto.(AS).
Jens-Petter Hauge
AC Milan wamewasilisha ofa ya kufungua ya euro milioni nne kwa winga wa Bodo/Glimt, Jens-Petter Hauge.
Hauge aliyavutia macho ya maofisa wa Rossoneri wakati wa pambano la kufuzu Ligi ya Europa huko San Siro juzi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifunga na kutoa msaada wakati wa kipigo cha 3-2 cha Bodo/Glimt, na Milan sasa wanataka makubaliano kabla ya soko la uhamisho kufungwa.(Calcio Mercato).
Jean-Clair Todibo
KLABU ya Everton wana azma ya kumchukuwa mlinzi wa Barcelona, Jean-Clair Todibo kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa.
‘The Toffees’ wanataka kupata huduma za yoso huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa mkopo mrefu, lakini, Barca itakubali tu mpango huo ikiwa jukumu la kununua litajumuishwa.(The Independent).
Ademola Lookman
FULHAM inakaribia kumsajili, Ademola Lookman kwa mkopo kutoka RB Leipzig.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikipiga Everton mapema katika soka yake, alijikuta akicheza mechi 10 tu za Bundesliga kwa Leipzig msimu uliopita.(Bild).
Alex Collado
YOSO wa Barcelona, Alex Collado yuko mbioni kuondoka Camp Nou.
Klabu za Porto na Sampdoria zinavutiwa na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, na ‘Blaugrana’ wapo tayari kuidhinisha kuondoka kwake kwa mkopo.(Marca).
Mario Balotelli
MSHAMBULIAJI mtukutu, Mario Balotelli, anaweza kuka njia yake ya juu Genoa, sambamba na beki wa Inter, Andrea Ranocchia.
Balotelli kwa sasa yuko chini ya mkataba na Brescia ya ‘Serie B’, lakini, Genoa wanataka kumlenga mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia na Ranocchia ili kusaidia kuipandisha timu kwenye jedwali.(Goal).