N’GOLO KANTE
MANCHESTER UNITED imewasiliana na washauri wa kiungo mkabaji wa Ufaransa N’Golo Kante kuhusu hatua ya kuondoka Chelsea, lakini makubaliano yoyote na mchezaji huyo, 29, huenda yakapelekea kupunguzwa pakubwa kwa mshahara wake wa pauni 300,000 kwa wiki. (Mirror)
JUAN MATA
LAZIO huenda ikataka kuwasajili viungo wawili wa Manchester United, Juan Mata, 32, na Mbrazili Andreas Pereira, 24. (Sun)
GLEISON BREMER
LEICESTER CITY wanapanga kumsajili beki wa kati wa Torino, 23, Mbrazili Gleison Bremer, ambaye pia anawindwa na klabu ya Everton. (Football Insider)
JOSHUA KING
MSHAMBULIAJI wa Bournemouth raia wa Norway Joshua King, 28 anawindwa na Tottenham Hotspur wakati huu ambapo klabu hiyo inataka kumsajili mshambuliaji kabla ya siku ya ukomo ya uhamisho. (Telegraph – subscription required)
USWIZI HARIS SEFEROVIC
SPURS pia wanapiga hesabu za kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Benfica na timu ya ya Uswizi Haris Seferovic, 28. (Football Insider)
ERIC GARCIA
MANCHESTER CITY wanatarajiwa kumuachia beki kinda Eric Garcia, 19, kurejea Barcelona endapo beki wa Benfica Ruben Dias akikubali kujikinga na Man City. (Sport – in Spanish)
JORGINHO,
PARIS ST-GERMAIN imekuwa ikiwasiliana na Chelsea juu ya kumsajili kwa mkopo kiungo wa Italia, Jorginho, 28. (Telefoot, via Mail)
VICTOR NELSSON
ASTON VILLA wametuma maombi ya usajili ya pauni milioni 9 kwa beki wa klabu ya Copenhagen Victor Nelsson, 21. (Ekstra Bladet – in Danish)
OLEKSANDR ZINCHENKO
MANCHESTER CITY wamewakaribisha Barcelona kumsajili Oleksandr Zinchenko, 23, ambaye anamudu kucheza kama beki ama winga wa kushoto. (Mundo Deportivo – in Spanish)
LAUTARO MARTINEZ
BARCELONA wameachana na mipango ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez, 23. (Calciomercato – in Italian)