Tariq Lamptey
MABINGWA wa Ujerumani, Bayern Munich wamewasiliana na Brighton juu ya uwezekano wa makubaliano na beki wa kulia, Tariq Lamptey (19). (Sport1).

Jadon Sancho
OFA ya Manchester United ya pauni milioni 91.3 kwa ajili ya mshambuliaji wa England, Jadon Sancho (20) imekataliwa na Borussia Dortmund. (Sky Sports).

Luka Jovic
MANCHESTER United pia wamejiunga na kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Real Madrid na Serbia, Luka Jovic (22), kwa mkopo. (AS).

Ousmane Dembele
MANCHESTER United inakaribia kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa, Ousmane Dembele (23), wakiipiga Barca jeki kifedha kumsajili mshambuliaji wa Lyon aliyekuwa Manchester United Memphis Depay. (AS).

David Alaba
KOCHA, Pep Guardiola anataka kumsajili beki wa kushoto mpya kabla ya dirisha kufungwa na David Alaba wa Bayern Munich na Austria, pamoja na mchezaji wa Ajax na Argentina, Nicolas Tagliafico, wote wakiwa na umri wa miaka 28, wakinyatiwa na Manchester City. (Mail).

Joey Veerman
KLABU ya Southampton huenda ikachukua hatua ya kuchelewa kumsajili kiungo wa Heerenveen ya Uholanzi, Joey Veerman. (Voetbal International).

Lucas Torreira
WAKALA wa Lucas Torreira amefika Madrid kufanya mazungumzo na Atletico Madrid juu ya uwezekano wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, raia wa Uruguay kuondoka Arsenal. (Fabrizio Romano).

Antonio Rudiger
CHELSEA iko tayari kumuuza mlinzi wa Ujerumani, Antonio Rudiger na ingawa Tottenham pia inamkodolea macho mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ingependelea ikiwa angehamia nchi za nje. (ESPN).

Thiago Silva
BEKI wa kulia wa Brazil, Thiago Silva (36), anasema alikasirishwa na vile Paris St-Germain ilivyoshughulikia kuondoka kwake, na hata ikiwa mabingwa hao wa Ufaransa waliomuongezea mkataba wa mwaka mmoja muda ulikuwa umekwenda kwasababu tayari alikuwa amekubali kujiunga na Chelsea. (ESPN).

Vladimir Coufal
OFA ya West Ham ya mkopo kwa beki wa kulia timu ya Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech, Vladimir Coufal (28), imekataliwa. (90min).

Santiago Arias
KLABU ya Everton ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Atletico Madrid na Colombia, Santiago Arias (28). (Liverpool Echo).

Alex Telles
MLINZI wa kushoto wa Porto, Alex Telles ana matumaini ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United ingawa klabu hizo hazijafikia makubaliano ya ada ya uhamisho kwa ajili ya Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 27. (Guardian).

Diogo Dalot
KLABU ya Manchester United imegoma kumuuza Diogo Dalot (21), kwenda Porto kama sehemu ya mpango wa kumnasa, Telles. (O Jogo).