NA ZAINAB ATUPAE

RAIS wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) Seif Kombo Pandu,amesema suala la kupata udhamini bado jinamizi kubwa linalowakabili hadi sasa.

Seif aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza na Zanzibar Leo.

Alisema Shirikisho limekuwa likipigana kutafuta udhamini huo lakini  bado hali inazidi kuwa ngumu.

“Tuhangaika kutafuta udhamini, tumekosa na hadi sasa hatujii kuna tatizo gani mpaka hali ikawa hivi”alisema.

Alisema udhamini wanao upata ni mdogo ambao hauwezi kukidhi mahitaji yote.

Hivyo aliwataka wafanya biashara kuendelea kushirikiana ili kupata udhamini kwa faida ya soka la Zanzibar.