KAMPALA,UGANDA
SPIKA wa Bunge la Uganda,Rebecca Kadaga amepongeza uhusiano wa kidugu uliopo baina ya nchi hiyo na Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran.
Spika alisisitiza kuwa,kuna umuhimu wa kuimarishwa zaidi uhusiano huo katika nyuga za uchumi,sayansi na teknolojia baina ya Kampala na Tehran.
Kadaga alisema hayo katika mazungumzo yake mjini Kampala na Morteza Mortazavi, Balozi wa Iran nchini Uganda.
Alisema kuhusu uhusiano mzuri wa kibunge ulioko baina ya Uganda na Iran na katika nyuga na taasisi za kimataifa kama vile Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na kubainisha kuwa, ushirikiano huo umejengeka katika misingi ya maslahi ya muda mrefu ya pande mbili.
Spika Kadaga wa Bunge la Uganda ameashiria kuhusu safari yake ya kuzitembelea Vyuo Vikuu vya Iran na kueleza bayana kuwa, fursa za namna hiyo zinapaswa kutumiwa vizuri zaidi.