KAMPALA,UGANDA

UGANDA imeyaamuru mashirika 208 ya kibinadamu yasitishe operesheni zao nchini humo kutokana na kukiuka kanuni kuhusiana na wakimbizi.

Waziri anayeshughulikia misaada, majanga na wakimbizi nchini Uganda Hilary Onek alisema,baadhi ya mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi isivyo halali kwenye kambi za wakimbizi, bila kusaini hati ya Maelewano na Ofisi ya Waziri Mkuu na bila vibali vya kufanya shughuli zao nchini Uganda.

Takwimu za Serikali zinaonesha kuwa ni asilimia 69 tu ya mashirika ya kibinadamu yamepata idhini ya kutoa misaada kwa wakimbizi nchini Uganda, ambayo ilipokea wakimbizi milioni 1.4 kutoka nchi jirani zikiwemo Sudan Kusini, DRC na Burundi.