KAMPALA,UGANDA
RAIS wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesema kwamba Serikali iko katika mchakato wa kupata vifaa vya uhakiki wa dijiti wa wapiga kura kwa kutumia data zao za biometriska kujaribu kuzuia wizi wa kura katika uchaguzi ujao.
“Imekuwa sehemu ya dhamira yangu tangu 1961 kuchangia kukomesha wizi wa kura nchini Uganda. Kwa hivyo, niliamua kuziba mianya hiyo pia. Njia pekee ya kuziba pengo hili ambayo haikutegemea umakini wa watu ilikuwa uhakiki wa wapiga kura kwa kutumia alama za vidole ili mpiga kura asajili mara moja tu,”alisema Rais Museveni .
Rais alisema timu ya mafisadi ambayo ilikuwa katika Tume ya Uchaguzi ilikataa kununua mfumo wa biometriska.
Mnamo Julai mwaka huu,maofisa wakuu nane wa Tume ya Uchaguzi, pamoja na katibu wa muda mrefu Sam Rwakojo,waliripotiwa kufutwa kazi kwa madai ya ufisadi unaohusiana na uchapishaji wa vifaa vya kura kwa uchaguzi wa 2021.
Alisema suala la rushwa, vitisho, mashambulizi, ni kwa Polisi na Umma kunasa ushahidi na wanashughulika na Wahalifu hao,hatua ambazo zingekomboa mchakato wa kupiga kura wa nchi kutoka kwa mafisadi.
Alisema chama chake, NRM, hakikuwa na rasilimali za kujenga mfumo wa dijiti kwa sababu walichagua kujipanga katika mchujo wa chama uliomalizika.
Museveni alishika madaraka akiwa kiongozi wa jeshi la waasi mnamo 1986 na waangalizi wengi wanasema wana shaka kuwa ataachana na madaraka kupitia uchaguzi wa kidemokrasia.