LONDON,UINGEREZA

BAADA  ya mazungumzo ya dharura mjini London, Umoja wa Ulaya umeonya kuwa mswada mpya wa Uingereza kuhusu biashara utakuwa ukiukaji mkubwa sana wa mpango wa Brexit.

Umoja wa Ulaya ulisema jaribio la Uingereza kutaka kuidhinisha Mswada wa Soko la Ndani, ambao utaweza kuipa nguvu za kuubadilisha mpango wa Brexit uliharibu kwa kiasi kikubwa uaminifu kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya ukiongeza kuwa ni jukumu la Uingereza kurejesha uaminifu huo.

Miongoni mwa maswala mengine, Umoja wa Ulaya unadai mswada huo mpya utahujumu kile kinachojulikana kama makubaliano ya Ijumaa Njema ambayo yalimaliza miongo kadhaa ya machafuko Ireland Kaskazini.