NA HAFSA GOLO

SHIRIKA la Bandari Zanzibar limesema hali ya uingiaji wa meli za kigeni  ndani ya bandari ya Malindi zinazobeba mizigo kutoka nje  umeanza kuimarika  mara baada ya maradhi ya corona kumalizika nchini.

Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa shirika hilo ,Juma Sururu Juma, alieleza hayo alipokua akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Malindi mjini Unguja.

Sururu alisema,ongezeko la uingiaji wa  kasi wa meli hizo bandarini hapo  unaendelea kustawi vyema    jambo ambalo limejenga matumaini katika shirika hilo kufikia  malengo ya ukusanyaji wa mapato waliokadiria katika mwaka  wa fedha 2020-2021.

Alisema jumla ya makontena 5,576 yameingia na kuhudumiwa kuanzia Juni hadi Agosti tangu kumalizika kwa maradhi hayo nchini ambapo kati ya makontena hayo 3,806 yalikuwa na uzito wa 20 ft  ambapo makontena 1,770 yalikuwa na ukubwa wa 40 ft.

Pamoja na mwamko huo wa uingiaji wa makontena nchini unaoendelea hata hivyo alisema ndani ya maradhi ya corona jumla ya makontena 6,993 yalihudumiwa.