NA ZAINAB ATUPAE

KLABU ya soka ya Umoja imefanikiwa kutinga fainali ya ligi daraja la pili wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja, baada ya kuifunga mabao 4-2 timu ya Small Banka.

Mchezo huo uliotimua vumbi majira ya saa 10:00 jioni,uliokuwa wa ushindani,huku kila timu ikisaka ushindi kwa uvumba na udi.

Mabao ya Umoja yalifungwa na Tahir Idd dakika ya 29 bao la pili liliongezwa na Suleiman Juma dakika ya 34, bao la tatu lilkafungwa na Maneno Hashir dakika ya 56 na Khamis Ali akahitimisha ushindi kwa bao la nne dakika ya 67.

Mabao ya Small Banka yaliwekwa wavuni na Abdalla Mohamed dakika ya 80 na 87.

Fainali ya mashindano hayo inatarajiwa kuchezwa Jumatano ambapo itapigwa leo Jumatano baina ya Umoja na Kimbani majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Dole.