WAPENZI wasomaji wetu leo hii nimewatayarishia tiba ya kutumia asali na mdalasini ambayo ni mjaraba kwa matatizo mengi mwilini mwa mwanaadamu.

Hivyo tumia huu ili kuepuka na kutibu magonjwa mbalimbali.

Manufaa ya Asali na Mdalasini:

ASALI  inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.

Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.

Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna faida  nyingi katika  asali na mdalasini kama ifuatayo:

1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.

Vinginevyo tengeneza chai kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.

Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja ‘cha chai’ cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73 yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

2. Kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu vijiko vitano vya asali, na kimoja cha mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.

Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

6. Lehemu {CHOLESTERAL}
Kipimo cha lehemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio} kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa gilasi  moja {ounce 16} yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki kutwa mara tatu kilifanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha lehemu mwilini.

Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhibitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dkt. Alexander Andreyed na Eric Vogelmann.

Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark Julai 1994. vilevile/ aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya lehemu.

7. Mafua {COLDS}
Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo.

8. Ugumba {INFERTILITY}
Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi kwa  wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa angalau vijiko viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}.

Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi ka kina mama wenye kuhitaji kuzaa.

Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.

10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.