NA ZUHURA JUMA, PEMBA
MASHEHA wa Shehia za Mkoa wa Kaskazini Pemba, wametakiwa kushirikiana na wazazi pamoja na walimu katika kuwalinda watoto dhidi ya maradhi mbali mbali ikiwemo ya kuambukiza.
Akiwasilisha mada namna ya kumlinda mtoto katika Ukumbi wa Halmashauri Wilaya ya Micheweni Pemba, Ofisa Uratibu Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Said Mohamed Said, aliyasema hayo katika Mkutano wa Masheha uliofadhiliwa chini ya UNICEF, alisema watoto wanahitaji kuongozwa, kulindwa na kujua haki zao.
Alisema kuwa, Masheha wana jukumu la kufuatilia na kushirikikikamilifu katika suala la kumlinda mtoto, ili kuwakinga na majanga mbali mbali ikiwemo maradhi ya kuambukiza kama Corona.
Alieleza kuwa, pamoja na kuwa Tanzania hakuna Corona, lakini ni vyemawakachukua tahadhari, ikiwa ni pamoja na kupita katika skuli zilizopo katika shehia zao kuhakikisha walimu wanazifuata taratibu zote
zilizowekwa na Serikali.“Kuna baadhi ya skuli hawafuati taratibu zilizowekwa katika kuwakinga watoto na ugonjwa wa corona, ingawa kwetu haupo lakini nchi jirani upo
na watu wanaingia kila siku, hivyo Masheha tuna jukumu la kufuatiliana kukagua”, alisema Ofisa huyo.