LONDON,UINGEREZA
UMOJA wa Mataifa na Uingereza kwa pamoja zinatarajiwa kuandaa mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabia nchi wa Desemba 12, ikiwa maadhimisho ya miaka minne ya makubaliano ya kihistoria kuhusu mazingira ya Paris.
Tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya Rais Xi Jinping wa China kuuambia Umoja wa Mataifa kwamba waharibifu wakubwa wa mazingira duniani wataweza kupunguza kwa kiwango cha uharibifu huo ifikapo 2030.
Ili kuendelea na jaribio la kuondosha kabisa gesi ya kaboni ifikapo 2060,hatua hiyo ilipokewa kwa shangwe na wanamazingira.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alisema hadi sasa tayari wana magwiji ya kukabiliana na hali hiyo karibu maeneo yote ya ulimwengu, pamoja na suluhisho lake na kwamba hakuna tena muda wa kupoteza katika suala la kuyatunza mazingira.
Ulimwengu bado upo katika jitihada ndogo ya kukabiliana na kupunguza kiwango cha joto duniani ambacho kimeongezeka kwa nyuzi joto 1.5.